Jeremiah 8:5-10


5 aKwa nini basi watu hawa walipotea?
Kwa nini Yerusalemu inapotea kila mara?
Wanang’ang’ania udanganyifu
na wanakataa kurudi.

6 bNimewasikiliza kwa makini,
lakini hawataki kusema lililo sawa.
Hakuna anayetubia makosa yake
akisema, “Nimefanya nini?”
Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewe
kama farasi anayekwenda vitani.

7 cHata korongo aliyeko angani
anayajua majira yake yaliyoamriwa,
nao njiwa, mbayuwayu na koikoi
hufuata majira yao ya kurudi.
Lakini watu wangu hawajui
Bwana anachotaka kwao.


8 d“ ‘Mwawezaje kusema, “Sisi tuna busara
kwa sababu tunayo sheria ya Bwana,”
wakati ambapo kwa hakika kalamu ya uongo ya waandishi
imeandika kwa udanganyifu?

9 eWenye hekima wataaibika,
watafadhaika na kunaswa.
Kwa kuwa wamelikataa neno la Bwana,
hiyo hekima waliyo nayo ni ya namna gani?

10 fKwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao,
na mashamba yao kwa wamiliki wengine.
Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,
wote wana tamaa ya kupata zaidi;
manabii na makuhani wanafanana,
wote wanafanya udanganyifu.
Copyright information for SwhKC